INDIA-USALAMA

Chama cha waziri mkuu nchini India chapoteza wafuasi wake Kashmir

Waziri Mkuu wa India Narendra Modi.
Waziri Mkuu wa India Narendra Modi. REUTERS/Adnan Abidi

Makada watatu wa chama cha Waziri Mkuu wa India Narendra Modi wameuawa Alhamisi wiki hii na wanaharakati wa Kashmir wanaotaka eneo hilo kuendelea kujitawala.

Matangazo ya kibiashara

Tukio hili linakuja siku chache baada ya serikali ya Narendra Modi kubadilisha kanuni zinazowaruhusu Wahindi wanaoishi katika maeneo mengine ya nchi kununua ardhi katika mkoa huu wa Himalaya.

Serikali imesema hii inakusudia kuweka Kashmir katika ardhi ya India kwa kutengeneza sheria sawa katika mikoa yote ya nchi.

Kashmir imendelea kukumbwa na machafuko tangu serikali kuu ya Modi mwaka jana kufuta uhuru wa kujitawala katika mkoa huu pekee wa Waislamu wengi nchini India, kabla ya kukamata viongozi kadhaa wa kisiasa wa eneo hilo ili kutuliza mzozo.

Eneo la Kashmir linapatikana India na Pakistan, lakini nchi hizo mbili zinalizozania kwa miaka kadhaa.