INDIA-CORONA-AFYA

Coronavirus: Zaidi ya kesi mpya 48,000 zathibitishwa nchini India

Idadi ya vifo vinavyotokana na Corona nchini India imeongezeka kutoka 563 katika muda wa saa 24 hadi 121,090, wizara imeongeza.
Idadi ya vifo vinavyotokana na Corona nchini India imeongezeka kutoka 563 katika muda wa saa 24 hadi 121,090, wizara imeongeza. REUTERS

India imerekodi visa vipya 48,648 vya maambukizi ya virusi vya Corona leo Ijumaa, na kufanya jumla ya visa vya maambukizi kufikia milioni 8.09, kulingana na takwimu zilizotolewa na Wizara ya Afya.

Matangazo ya kibiashara

Kwa idadi ya visa vya maambukizi, India inaendelea kusalia nyuma ya Marekani (karibu visa milioni 9 vya maambukizi) katika orodha ya nchi zilizoathirika zaidi na janga hilo.

Idadi ya visa vya kila siku vya maambukizi vimepungua hivi karibuni lakini wataalam wanahofu kuanza tena kusambaa kwa virusi hivyo baada ya kuingia kwa kipindi cha sherehe kuu za dini la Kihindu, ambazo zinatarajiwa kudumu hadi katikati ya mwezi Novemba.

Idadi ya vifo vinavyotokana na Corona nchini India imeongezeka kutoka 563 katika muda wa saa 24 hadi 121,090, wizara imeongeza.