UTURUKI-MAJANGA ASILIA

Tetemeko la ardhi: Uturuki yaendelea na zoezi la kutafuta miili ya waliofariki dunia

Shughuli za uokoaji zinaendelea leo Jumatatu nchini ya vifusi vya majengo manane huko Izmir, mji ulio magharibi mwa Uturuki, wakati idadi ya waliofariki dunia kutokana na tetemeko la ardhi lenye nguvu lililopiga eneo la Aegean imefikia 81.

Zaidi ya mahema 3,500 na vitanda 13,000 vya muda vimewekwa sehemu maalum, kulingana na idara ya usimamizi wa majanga nchini Uturuki, ambalo limeripoti watu 962 wamejeruhiwa.
Zaidi ya mahema 3,500 na vitanda 13,000 vya muda vimewekwa sehemu maalum, kulingana na idara ya usimamizi wa majanga nchini Uturuki, ambalo limeripoti watu 962 wamejeruhiwa. REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Awali mamlaka nchini Uturuki ilisema watu 79 walfariki dunia huko Izmir na vijana wawili waliuawa katika kisiwa cha Ugiriki cha Samos.

Zaidi ya mahema 3,500 na vitanda 13,000 vya muda vimewekwa sehemu maalum, kulingana na idara ya usimamizi wa majanga nchini Uturuki, ambalo limeripoti watu 962 wamejeruhiwa.

Sehemu kubwa ya watu waliojeruhiwa, zaidi ya 740, waliruhusiwa kutoka hospitali, idara ya usimamizi wa majanga nchini Uturuki imebaini.