Coronavirus: Visa vipya 17 vyathibitisha China
China imerekodi visa vipya 17 vilivyothibitishwa vya maambukizi ya virusi vya Corona katika muda wa saa ishirini na nne zilizopita, mamlaka ya afya imetangaza leo Jumatano.
Imechapishwa:
Katika taarifa, Tume ya Kitaifa ya Afya imesema visa 15 vinahusu watu wanaliongia nchini humo wakitokea nchi za kigeni.
Kulingana na takwimu zilizochapishwa katika ripoti yake ya kila siku juu ya janga hilo, visa 86,087 vya maambukizi ya virusi vya Corona vimethibitishwa katika China bara.
Janga la Corona limesababisha vifo vya watu 4,634 nchini China. Hakuna vifo vpya vilivyoripotiwa leo Jumatano.
Mlipuko wa virusi vya corona unaosababisha ugonjwa wa COVID-19, ulitokea katika mkoa wa Hubei nchini China mwishoni mwa mwaka 2019.
Kufikia sasa kinachojulikana ni kuwa COVID-19, ni ugonjwa ambao unaothiri mfumo wa kupumua wa binadamu.
Dalili zake ni pamoja na homa kali, kukohoa ambako baada ya wiki moja muathiriwa anakabiliwa na tatizo la kupumua.