Coronavirus: China yarekodi visa vipya 33 vya maambukizi
Visa vipya 36 vipya vya maambukizi ya virusi vya Corona vimethibitishwa nchini china katika muda wa saa ishirini na nne zilizopita, mamlaka ya afya imeripoti leo Jumatatu.
Imechapishwa:
Katika taarifa, Tume ya Kitaifa ya Afya imesema visa 32 vinahusu watu waliotokea katika nchi za kigeni.
Kulingana na takwimu zilizochapishwa katika ripoti yake ya kila siku juu ya janga hilo, visa 86,245 vya maambukizi ya virusi vya Corona vimethibitishwa katika China bara.
Janga la COVID-19 limesababisha vifo vya watu 4,634 nchini China. Hakuna vifo vipya vilivyoripotiwa leo Jumatatu.
Mlipuko wa virusi vya corona unaosababisha ugonjwa wa COVID-19, ulitokea katika mkoa wa Hubei nchini China mwishoni mwa mwaka 2019.
Kufikia sasa kinachojulikana ni kuwa COVID-19, ni ugonjwa ambao unaothiri mfumo wa kupumua wa binadamu.