GEORGIA-SIASA-USALAMA

Georgia: Makumi ya maelfu ya waandamanaji wadai uchaguzi mpya

Waandamanaji walifurika kwenye barabara kuu ya Tbilisi
Waandamanaji walifurika kwenye barabara kuu ya Tbilisi AFP

Makumi ya maelfu ya wafuasi wa upinzani wamejitokeza mitaani huko Georgia siku ya Jumapili kudai uchaguzi mpya wa wabunge, wakituhumu mamlaka kwa wizi wa kura ambapo chama tawala kimeibuka mshindi wa uchaguzi huo kwa kupata viti vingi.

Matangazo ya kibiashara

Polisi wa kuzuia ghasia katika jimbo la Georgia, ambao walitumia maji ya kuwasha dhidi ya waandamanaji, waliingilia kati wakati waandamanaji hao walitishia kuzuia jengo la Tume ya Uchaguzi ya Georgia.

"Natoa wito kwa wale ambao wanashiriki katika mikusanyiko hii iliyopigwa marufuku wajiepushe na kitendo chochote kilichopigwa marufuku," kiongozi wa chama tawala Irakli Kobakhidze amesema katika mkutano wa usiku na waandishi wa habari.

"Wahalifu watakuwa gerezani hivi karibuni," ameongeza, akimaanisha viongozi wa upinzani.

Waandamanaji walifurika kwenye barabara kuu ya Tbilisi. Vyanzo rasmi vinabaini kwamba takriban waandamanaji 45,000 walikusanyika nje ya bunge, wengi wao wakiwa wamevalia vifaa barakoa kwa kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona wakati nchi hiyo kama inaendelea kukabiliwa na janga la COVID-19.