ARMENIA-AZERBAIJAN-URUSI-USALAMA

Nagorno-Karabakh: Armenia na Azerbaijan zasaini mkataba wa kusitisha vita

Dakika chache baada ya tangazo kama hilo kutoka kwa Waziri Mkuu wa Armenia, rais wa Urusi Vladimir Putin amethibitisha mkataba wa kudumu wa "kusitisha mapigano" kati ya Armenia na Azerbaijan kwa mkoa wa Nagorno-Karabakh.

Waarmenia wakikusanyika mbele ya makao makuu ya serikali, usiku wa Novemba 9 kuamkia 10, 2020.
Waarmenia wakikusanyika mbele ya makao makuu ya serikali, usiku wa Novemba 9 kuamkia 10, 2020. Karen MINASYAN / AFP
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Urusi ameongeza kwamba mkataba huo umeanza kutekelezwa tangu saa tatu usiku Jumatatu wiki hii.

Baada ya mapigano ya wiki sita huko Nagorno-Karabakh, Azerbaijan na Armenia wmetia saini mkataba kamili wa kusitisha mapigano. "Mnamo Novemba 9, rais wa Azerbaijan (Ilham Aliev), Waziri Mkuu wa Armenia (Nikol) Pashinian na Rais wa Urusi wametia saini tangazo la kusitisha mapigano na kusitishwa kwa vitendo vyote vya kijeshi katika eneo la kivita la Nagorno-Karabakh kuanzia saa sita usiku Novemba 10 saa za Moscow, ”Vladimir Putin amesema katika taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari.

Nakala hiyo, iliyochapishwa jioni, haibaini tuusitishwaji wa uhasama lakini pia inafafanua misingi ya suluhu ya kisiasa ya mzozo wa Nagorno-Karabakh, mwandishi maalumu wa France Médias Monde, Régis Genté, ameripoti. Nakala hiyo inaagiza kutumwa kwa kikosi cha askari karibu 2,000 wa urusi, askari na walinzi wa mipakani ili kuhakikisha mapigano yamesitishwa kwenye eneo maalumu linalounganisha nchi hizo mbili na eneo linaloitwa Lachine, na kuondoka kwa vikosi vya Armenia. Wanajeshi wanatarajiwa kukaa hapo kwa miaka mitano, kipindi ambacho kinaweza kuongezwa tena kwa miaka mingine mitano.