ARMENIA-AZERBAIJAN--USALAMA

Karabakh: Uturuki kutuma wanajeshi wake kusimamia makubaliano ya usitishaji mapigano

Azerbaijan na Armenia zilishindwa kudumisha mara mbili makubaliano ya usitishaji mapigano yaliyopatanishwa na Urusi. Jumla ya vifo kwa pande zote mbili imezidi 1,000.
Azerbaijan na Armenia zilishindwa kudumisha mara mbili makubaliano ya usitishaji mapigano yaliyopatanishwa na Urusi. Jumla ya vifo kwa pande zote mbili imezidi 1,000. AP Photo

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan ameomba idhini ya Bunge kutuma wanajeshi wa nchi hiyo nchini Azerbaijan kushiriki katika ujumbe wa kusimamia makubaliano ya usitihaji mapigano unaoundwa na Urusi na Uturuki huko Nagorno-Karabakh, kwa mujibu wa shirika la habari la AFP.

Matangazo ya kibiashara

Baada ya mapigano ya wiki sita huko Nagorno-Karabakh, Azerbaijan na Armenia walitia saini kwenye mkataba kamili wa usitishaji mapigano Novemba 9, 2020.

Azerbaijan na Armenia zimesaini makubaliano ya kusitisha mapigano kwa ushirikiano wa rais wa Urusi Vladimir Putin.

Azerbaijan na Armenia zilishindwa kudumisha mara mbili makubaliano ya usitishaji mapigano yaliyopatanishwa na Urusi. Jumla ya vifo kwa pande zote mbili imezidi 1,000.

Waangalizi wanafuatilia kuona ikiwa nchi hizo mbili zitaheshimu makubaliano ya kusitisha mapigano.