KOREA KUSINI-CORONA-AFYA

Coronavirus: Korea Kusini yaongeza hatua za kukabiliana na Corona

Korea Kusini imeamua kuongeza vizuizi vya kiafya katika mji mkuu wa Seoul na viunga vyake kutokana na ongezeko vida vya maambukizi mapya ya Corona vilivyorekodiwa kila siku, Waziri Mkuu Chung Sye-kyun amesema leo Jumanne.

Operesheni ya kunyunyuzia dawa kuzuia kuenea kwa virusi vya Corona katika trni ya mwendo kazi , Seoul, Machi 12, 2020.
Operesheni ya kunyunyuzia dawa kuzuia kuenea kwa virusi vya Corona katika trni ya mwendo kazi , Seoul, Machi 12, 2020. YONHAP / AFP
Matangazo ya kibiashara

Hatua hizo kali ni pamoja na kupiga marufuku mikusanyiko ya watu zaidi ya 100, kupunguza idadi ya watu wanaohudhuria ibada mbalimbali kanisani na katika matukio ya michezo hadi 30% ya uwezo wa ukumbi, wakati watu wametakiwa kutokaribiana kwa umbali wa mita moja katika sehemu zinazojulikana kama zenye hatari kama vilabu vya usiku na baa.

Korea Kusini ambayo ni nchi ya kwanza nje ya China kukumbwa na janga la corona baada ya kuzuka nchini humo, ni moja ya nchi ambazo zimefaulu vizuri kudhibiti mgogoro huu wa kiafya, kupitia kampeni kubwa za vipimo na kufuatilia watu waliotangamana na wagonjwa wa COVID-19.

Serikali imeamua kuongeza hatua baada ya jumla ya kesi mpya zilizothibitishwa nchini kuzidi 200 Jumatatu kwa siku ya tatu mfululizo, ikiwani kiwango kikubwa zaidi tangu mapema mwezi Septemba.

Karibu nusu ya watu milioni 52 wa Korea Kusini wanaishi katika mkoa wa Seoul.