Coronavirus: Vifo vya kila siku nchini Urusi vyaendelea kuongezeka
Urusi imetangaza leo Jumanne idadi ya rekodi ya vifo 442 vilivyosababishwa na virusi vya Corona, na kusababisha idadi rasmi ya vifo kufikia 33,931.
Imechapishwa:
Mamlaka pia nchini humo imerekodi visa vipya 22,410 vya maambukizi ya virusi hivyo katika muda wa saa 24 zilizopita, ikiwa ni pamoja na visa 5,882 katika mji mkuu Moscow, na kufanya jumla ya maambukizi nchi nzima kufikifia 1,971,013.
Ongezeko la maambukizi mapya limeendelea kuripotiwa katika nchi mbalimbali barani Ulaya, katika baadhi ya nchi za Amerika na Asia.
Mlipuko wa virusi vya corona unaosababisha ugonjwa wa Covid-19, ulitokea katika mkoa wa Hubei nchini China mwishoni mwa mwaka 2019.
Kufikia sasa kinachojulikana ni kuwa Covid-19, ni ugonjwa ambao unaothiri mfumo wa kupumua wa binadamu.
Dalili zake ni pamoja na homa kali, kukohoa ambako baada ya wiki moja muathiriwa anakabiliwa na tatizo la kupumua.