CHINA-CORONA-AFYA

Coronavirus: Visa vipya 17 vya maambukizi vyathibitishwa China

Kulingana na takwimu kutoka tume hiyo, visa 86,398 vya maambukizi ya virusi vya Corona vimethibitishwa katika China Bara.
Kulingana na takwimu kutoka tume hiyo, visa 86,398 vya maambukizi ya virusi vya Corona vimethibitishwa katika China Bara. STR / AFP

China imerekodi visa vipya 17 vya maambukizi ya virusi vya Coreona vilivyothibitishwa katika muda wa saa ishirini na nne zilizopita, mamlaka ya afya imebaini leo Ijumaa.

Matangazo ya kibiashara

Katika taarifa, Tume ya kitaifa ya afya imebaini kwamba visa hivi vyote vinahusu watu walioingia nchini kutoka nchi za kigeni hivi karibuni.

Kulingana na takwimu kutoka tume hiyo, visa 86,398 vya maambukizi ya virusi vya Corona vimethibitishwa katika China Bara.

Janga la Corona limesababisha vifo vya watu 4,634 nchini China. Hakuna vifo vipya ambavyo vimevyoripotiwa leo Ijumaa.