ARMENIA-URUSI-AZERBAIJAN-USALAMA-USHIRIKIANO

Armenia yataka kuimarisha ushirikiano wa kijeshi na Urusi

Waziri Mkuu wa Armenia Nikol Pachinian.
Waziri Mkuu wa Armenia Nikol Pachinian. Armenian Prime Minister Press Service/Tigran Mehrabyan/PAN Photo

Waziri Mkuu wa Armenia Nikol Pachinian ameomba kuimarishwa kwa uhusiano wa kijeshi kati ya nchi yake na Urusi. Tamko hili linakuja chini ya wiki 2 baada ya jeshi lake kushindwa katika mgogoro wa Nagorno-Karabakh na Azerbaijani, ambayo imeendelea kudhibiti baadhi ya maeneo ya jimbo hilo.

Matangazo ya kibiashara

Baada ya makubaliano ya Novemba 9, yaliyotiwa saini chini ya mwavuli ya rais wa Urusi Vladimir Putin, karibu walinda amani 2,000 wa Urusi walipelekwa huko Karabakh.

"Tuna imani kuwa tunaweza kuimarisha ushirikiano na Urusi sio tu katika nyanja ya usalama, bali pia katika ushirikiano wa kijeshi na kiufundi. Ni kwa maneno haya, Nikol Pachinian amekaribisha ziara ya Mawaziri wa Ulinzi na Mambo ya nje wa Urusi, Bibi Shoïgou na Lavrov jijini Yerevan.

Haya ndio mambo yanayotosheleza Urusi, ambayo tayari ina kambi mbili za jeshi huko Armenia na ambayo hivi karibuni ilipeleka wanajeshi 2,000 katika eneo la Nagorno-Karabakh, ambalo Baku inachukulia kama eneo lake.