MAREKANI-TAIWAN-USHIRIKIANO

Afisa wa juu katika jeshi la Marekani ziarani Taiwan, China yaghadhabishwa

Gazeti la United Daily News la Taiwan limechapisha picha za ndege ya kibinafsi iliyotajwa kama ndege ya jeshi la Marekani wakati afisa huyo wa jeshi la Marekani aliwasili kwenye Uwanja wa ndege wa Songshan katikati mwa jiji la Taipei.
Gazeti la United Daily News la Taiwan limechapisha picha za ndege ya kibinafsi iliyotajwa kama ndege ya jeshi la Marekani wakati afisa huyo wa jeshi la Marekani aliwasili kwenye Uwanja wa ndege wa Songshan katikati mwa jiji la Taipei. REUTERS

Michael Studeman, mkuu wa kikosi cha wanamaji cha Marekani, kilichobobea katika ujasusi wa kijeshi katika eneo la Asia-Pacific, amefanya ziara ya kushtukiza huko Taiwan, vyanzo viwili vimesema kulingana na shirika la habari la REUTERS, hatua ambayo inaweza kuighadhabisha China.

Matangazo ya kibiashara

Pentagon ilmekataa kujieleza. Wizara ya Mambo ya nje ya Taiwan imethibitisha kwamba afisa wa ngazi ya juu katika jeshi la Marekani amewasili kwenye kisiwa hicho lakini haikutoa maelezo zaidi, ikiongeza kuwa safari hiyo haikuwekwa wazi kwa umma.

China, ambayo inadai Taiwan kama eneo lake, ilijibu kwa hasira kuhusu ziara ya Waziri wa Afya wa Marekani Alex Azar huko Taipei mwezi Agosti mwaka huu na baadaye kuhusu ziara ya Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Keith Krach mwezi Septemba. Beijing ilikuwa kila wakati ikipeleka ndege za kivita karibu na kisiwa hicho.

Utawala wa Trump umeongeza uungwaji wake mkono kwa Taiwan, hasa kwa kuiuzia silaha, bila idhini kutoka mamlaka ya China.

Gazeti la United Daily News la Taiwan limechapisha picha za ndege ya kibinafsi iliyotajwa kama ndege ya jeshi la Marekani wakati afisa huyo wa jeshi la Marekani aliwasili kwenye Uwanja wa ndege wa Songshan katikati mwa jiji la Taipei.

Takwimu kutoka planefinder tovuti ya ufuatiliaji wa safari za ndege, zinaonyesha kuwasili kwa ndege ya kibinafsi kutoka Hawaii - kunakopatikana makao makuu ya jeshi la Marekani katika ukanda wa India-Pacific - kwa Uwanja wa ndege wa Songshan Jumapili alasiri, muda mfupi kabla ya picha hizo kuwekwa kwenye tovuti ya Gazeti lma United Daily News.