URUSI-CORONA-AFYA

Coronavirus: Watu 491 wafariki dunia kutokana na Corona katika muda wa saa 24 nchini Urusi

Sampuli za chanjo ya corona iliyotengenezwa na Taasisi ya Utafiti ya Gamaleya, huko Moscow, Urusi, Agosti 6, 2020.
Sampuli za chanjo ya corona iliyotengenezwa na Taasisi ya Utafiti ya Gamaleya, huko Moscow, Urusi, Agosti 6, 2020. The Russian Direct Investment Fund (RDIF)/Handout via REUTERS

Urusi imerekodi vifo 491 vilivyotokana na ugonjwa hatari wa COVID-19 kwa jumla ya vifo 37,031 tangu kuzuka kwa janga hilo nchini humo.

Matangazo ya kibiashara

Mamlaka ya afya pia imeripoti visa vipya 24,326 vya maambukizi ya virusi vya Corona katika muda wa saa 24, ikiwa ni pamoja na visa 5,838 katika mji mkuu wa Moscow, na kufanya idadi ya visa vilivyothivitishwa kufikia 2,138,828 nchini humo.

Hivi karibuni watafiti wamesema chanjo dhidi ya virusi vya Corona iliyotengenezwa na Chuo Kikuu cha Oxford nchini Uingereza, ina uwezo wa kuzuia watu kupata dalili za maambukizi ya virusi hivyo kwa kiasi kikubwa baada ya kumalizika kwa majaribio kuhusu uwezo wa chanjo hiyo.

Mlipuko wa virusi vya corona unaosababisha ugonjwa wa Covid-19, ulitokea katika mkoa wa Hubei nchini China mwishoni mwa mwaka 2019.

Kufikia sasa kinachojulikana ni kuwa Covid-19, ni ugonjwa ambao unaothiri mfumo wa kupumua wa binadamu.

Dalili zake ni pamoja na homa kali, kukohoa ambako baada ya wiki moja muathiriwa anakabiliwa na tatizo la kupumua.