CHINA-JAPANI-USHIRIKIANO

Waziri wa mambo ya nje wa China ziarani Japan

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi.
Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi. REUTERS / CHINA DAILY

Waziri wa Mambo ya nje wa China anatarajia kuzuru Japan leo Jumanne, ambapo atafanya ziara ya kwanza na mwakilishi wa ngazi ya juu wa China tangu Japani ilipopata waziri mkuu mpya mwezi Septemba wakati wasiwasi ukiongezeka kuhusu matarajio ya eneo la Beijing katika kanda hiyo.

Matangazo ya kibiashara

Wang Yi wakati huo atatoa wito kwa Waziri Mkuu wa Japan Yoshihide Suga, ambaye ametaka kuwepo na usawa kati ya utegemezi wa uchumi wa Japani kwa China na maswala ya usalama, pamoja na madai ya eneo la Beijing, katika Bahari ya Kusini mwa China.

Ziara hii ya waziri wa mambo ya nje wa China, mpinzani wa Marekani, ambayo ni mshirika wa Japan inakuja wakati Marekani mapema wiki hii afisa wa juu katika jeshi la Marekani alifanya ziara katiak kisiwa cha Taiwan.

Michael Studeman, mkuu wa kikosi cha wanamaji cha Marekani, kilichobobea katika ujasusi wa kijeshi katika eneo la Asia-Pacific, alifanya ziara ya kushtukiza huko Taiwan, vyanzo viwili vilisema kulingana na shirika la habari la REUTERS, hatua ambayo inaweza imeighadhabisha China.

Yoshihide Suga amechukua hatua za kupunguza ushawishi wa Beijing kwa kuimarisha uhusiano wa Tokyo na Australia na kufanya ziara nchini Vietnam na Indonesia.

"Kuna maswala tofauti kati ya nchi hizi mbili, kwa hivyo ni muhimu, kupitia mikutano ya kiwango cha juu, kupata suluhisho kwa kila suala moja kwa moja," Toshimitsu Motegi, Waziri wa Mambo ya Nje wa Japan, aliwaambia waandishi wa habari Jumatatu wiki hii, akiongeza kuwa atakuwa na "mazungumzo" na mwenzake wa China.

Wang Yi amepanga kuzuru Korea Kusini baadaye, kwa mazungumzo ambayo Korea Kaskazini itashirikishwa.