URUSI-INDIA

Coronavirus: India kutengeneza sehemu ya chanjo ya Urusi Sputnik V

Wafanyakazi wa afya nchini India wakichukua vipimo vya COVID-19 kwa raia wa nchi hiyo tarehe  29, Agosti 2020.
Wafanyakazi wa afya nchini India wakichukua vipimo vya COVID-19 kwa raia wa nchi hiyo tarehe 29, Agosti 2020. © Anupam Nath/AP Photo

Shirika la Fedha la Urusi na kampuni ya kutengeneza dawa ya Hetero nchini India, wamefikia makubaliano ya kutengeneza nchini India dozi milioni 100 ya chanjo ya Sputnik V dhidi ya COVID-19 kwa mwaka, kulingana na shirika la habari la Reuters.

Matangazo ya kibiashara

Kampuni ya Hetero na Mfuko wa Uwekezaji wa moja kwa moja wa Urusi, ambao umefadhili kutengenezwa kwa chanjo hiyo na ambayo inahusika na uuzaji wake duniani, wanapanga kuanza kutengeneza mapema mwaka 2021.

 

Majaribio ya kliniki ya Awamu ya II na III yanaendelea nchini India. Maabara ya Dr Reddy nchini India inasema inasema kuwa vipimo kamili vitakamilika mnamo mwezi Machi 2021.

 

Urusi na India zimeendelea kuelemewa na ugonjwa hatari wa COVID_19 unaosababishwa na virusi vya Corona tangu kuzu katika nchi hizo na sasa zimeanza kushuhudia wimbi jipya la maambukizi ya virusi vya Corona.