CHINA-CORONA

Coronavirus: Visa vipya 5 vyathibitishwa China

Baada ya miezi mitatu ya kupungua kwa visa vya maambukizi, tangu kiwango cha juu kama hicho kufikiwa mwishoni mwa mwezi Julai, idadi ya kila siku ya maambukizi imeongezeka tena nchini Brazil.
Baada ya miezi mitatu ya kupungua kwa visa vya maambukizi, tangu kiwango cha juu kama hicho kufikiwa mwishoni mwa mwezi Julai, idadi ya kila siku ya maambukizi imeongezeka tena nchini Brazil. REUTERS

China imerekodi visa vipya 5 vilivyothibitishwa vya maambukizi ya virusi vya Corona katika muda wa saa ishirini na nne zilizopita, mamlaka ya afya imebaini leo Ijumaa.

Matangazo ya kibiashara

Katika taarifa, Tume ya kitaifa ya Afya imesema kwamba visa vyote vinahusu watu wanaowasili nchini humo kutoka nchi za kigeni.

 

Kulingana na data kutoka Tume ya kitaifa ya Afya, visa 86,495 vya maambukizi ya virusi vya Corona vimethibitishwa katika China Bara.

 

Ugonjwa wa COVID-19 unaosababishwa na virusi vya Corona umesababisha vifo vya watu 4,634 nchini China. Hakuna vifo vipya ambavyo vimeripotiwa leo Ijumaa, kulingana na Tume ya kitaifa ya Afya.