URUSI-NATO

Urusi kushiriki mazoezi ya vikosi vya majini pamoja na NATO

Bendera ya NATO
Bendera ya NATO REUTERS/Francois Lenoir

Jeshi la Wanamaji la Urusi limesema Alhamisi kwamba meli zake zitashiriki, kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka kumi, katika mazoezi pamoja na NATO, ambayo yatahusisha nchi zaidi ya 30 kutoka pwani ya Pakistan.

Matangazo ya kibiashara

Mazoezi ya kupambana na uharamia yayanayojulikana kama AMAN-2021 yatafanyika katika bahari karibu na mji wa Karachi mwezi wa Februari 2021 na yatajumuisha, kati ya wengine, vikosi vya BUingereza, Marekani, Uturuki, China na Japani, Wizara ya Ulinzi ya Urusi imesema katika taarifa.

Urusi imepanga kutuma meli kubwa ya kivita, meli ya doria, helikopta yenye uwezo wa kufanya kazi majini na vitengo vingine, imesema kwenye wavuti yake.

Meli za jeshi la majini la Urusi na NATO zilikuwa hazijafanya kazi pamoja tangu mazoezi ya Bold Monarch yaliyoendeshwa na NATO mnamo mwaka 2011 katika pwani ya Uhispania, kulingana na shirika la habari la Urusi Tass.

Uhusiano kati ya Urusi na nchi za Magharibi si mzuri tangu kumalizika kwa vita Baridi, ukisababishwa hasa na uamuzi wa Urusi wa kuunganisha jimbo la Crimea la Ukraine kwenye ardhi yake mnamo mwaka 2014