YEMEN-SAUDI ARABIA

Yemen: Serikali na wanaharakati wanaotaka kujitenga watekeleza mkataba wa Riyadh

Mojawapo ya mji wa Yemen ulioharibiwa kutokana na vita
Mojawapo ya mji wa Yemen ulioharibiwa kutokana na vita REUTERS/Khaled Abdullah

Muungano wa kijeshi unaoongozwa na Saudi Arabia nchini Yemen umesema utekelezaji wa mkataba wa Riyadh wenye lengo la kuwaleta pamoja washirika wake kutoka Yemen utaanza siku ya Alhamisi.

Matangazo ya kibiashara

Kulingana na duru za kuaminika  utekelezaji huo utaanza kwa kupelekwa kwa wanajeshi Kusini mwa nchi kabla ya kutangazwa kwa zoezi jipya la kugawana madaraka.

Mkataba huo uliofikiwa mwishoni mwa mwaka huu utatekemezwa ili kuleta pamoja Baraza la mpito la Kusini na serikali, pande mbili ambazo zenye uhusiano mgumu licha ya kuwa zinapigana dhidi ya waasi wa Houthi katika mzozo ambao umekuwa ukiathiriYemen kwa zaidi ya miaka mitano.

Muungano wa kijeshi unaoongozwa na  Saudia umesema katika taarifa kwamba utaanza kusimamia zoezi jipya la kugawana madaraka katika mkoa wa Abyan siku ya Alhamisi, ukibaini kwamba makubaliano yalifikiwa juu ya kuundwa kwa baraza jipya la mawaziri 24, ambapo wanaharakati wanaotaka kujitenga kutoka Kusini mwa nchi watashirikishwa.

Mgogoro huu, unaochukuliwa katika ukanda huo kama vita vya kati ya Saudi Arabia na Iran, umesababisha vifo vya watu zaidi ya 100,000 na kusababisha kile Umoja wa Mataifa unachukulia kama mzozo mbaya zaidi wa kibinadamu duniani.

Waasi wa Kishia wa Houthi, ambao wameshikilia mji mkuu wa Yemen na vituo vikuu vya miji tangu mwishoni mwa 2014, wanasema wanapambana na mfumo mbovu unaojihusisha na ufisadi.