HONG KONG-SIASA-DEMOKRASIA

Tajiri wa Hong Kong Jimmy Lai ashtakiwa chini ya sheria mpya ya usalama wa kitaifa

Jimmy Lai, mwanaharakati wa Demokrasia katika eneo la Hong Kong
Jimmy Lai, mwanaharakati wa Demokrasia katika eneo la Hong Kong AP

Jimmy Lai, Mmiliki wa kampuni ya habari ”Next Digital” na mtu mashuhuri katika harakati za kupigania demokrasia, ameshtakiwa kwa tuhuma ya kushirikiana na vikosi vya kigeni na kuhatarisha usalama wa kitaifa, Gazeti la kila siku la Apple Daily limeripoti, likinukuu chanzo cha polisi.

Matangazo ya kibiashara

Lai, mkosoaji mkubwa wa Beijing, ndiye mtu wa kwanza mashuhuri kushtakiwa chini ya sheria mpya ya usalama.

Sheria ya usalama wa kitaifa iliyowekwa mnamo mwezi Juni mwaka huu katika koloni hili la zamani la Uingerezai inaadhibu kile Beijing inaona kama harakati za kujitenga, uasi, ugaidi na kushirikiana na nchi za kigeni.

Mapema mwezi huu, Jimmy Lai mwenye umri wa miaka 73 alikataliwa ombi la dhamana kwa madai ya udanganyifu kuhusiana na kukodisha mali isiyohamishika kwenye majengo ya Apple Daily.