JAPAN-CORONA-AFYA

Coronavirus: Zaidi ya visa bipya 3,000 vyathibitishwa Japani

Gari la kubeba wagonjwa wa Covid 19
Gari la kubeba wagonjwa wa Covid 19 AP Photo/Pavel Golovkin

Japani kwa mara ya kwanza imerekodi visa vipya 3,041vya maambukizi ya virusi vya Corona vinavyosababisha ugonjwa hatari wa COVID-19, redio na runinga vya serikali vimeripoti.

Matangazo ya kibiashara

Japani iko mbali kupata kiwango cha maambukizi sawa na nchi za Ulaya au Marekani, lakini msimu wa baridi unaonekana kurahisisha kusambaa kwa janga hilo nchini Japan, hasa katika mikoa ya kaskazini kama kisiwa cha Hokkaido. .

Ugonjwa wa COVID-19 umeua watu 2,588 hadi sasa nchini Japan.

Mlipuko wa virusi vya corona unaosababisha ugonjwa wa COVID-19, ulitokea katika mkoa wa Hubei nchini China mwishoni mwa mwaka 2019.

Kufikia sasa kinachojulikana ni kuwa COVID-19, ni ugonjwa ambao unaothiri mfumo wa kupumua wa binadamu.

Dalili zake ni pamoja na homa kali, kukohoa ambako baada ya wiki moja muathiriwa anakabiliwa na tatizo la kupumua.