SAUDI ARABIA

Covid 19: Saudi Arabia yaanza kutoa chanjo ya Pfizer

Janga la Covid 19
Janga la Covid 19 Radoslav Zilinsky/Getty Images

Saudi Arabia imeanza kutoa dozi za kwanza za chanjo ya Corona kwa raia wake, na kuwa nchi ya kwanza ya Kiarabu kutumia chanjo ya Pfizer-BioNTech, ambapo shehena mbili za dawa ziliwasili nchini humo Jumatano wiki hii.

Matangazo ya kibiashara

Awamu ya kwanza ya mpango wa chanjo itahusu kulinda wale walio katika hatari zaidi ya ugonjwa huo, na hatua mbili zitakazofuata zitahusu watu wenye umri wa zaidi ya miaka 50 kabla ya chanjo hiyo kutolewa kwa umma katika nchi hii ambayo imerekodi visa 360,000 vya maambukizi na vifo 6,080 tangu kuzuka kwa janga hilo.

Vituo vya chanjo vitawekwa kote nchini Saudi Arabia, amesema Waziri wa Afya Tawfiq Al-Rabiah, ambaye alikuwa mmoja wa watu wa kwanza kupokea chanjo hiyo nchini.

Mlipuko wa virusi vya Corona unaosababisha ugonjwa wa COVID-19, ulitokea katika mkoa wa Hubei nchini China mwishoni mwa mwaka 2019.

Kufikia sasa kinachojulikana ni kuwa COVID-19, ni ugonjwa ambao unaothiri mfumo wa kupumua wa binadamu.

Dalili zake ni pamoja na homa kali, kukohoa ambako baada ya wiki moja muathiriwa anakabiliwa na tatizo la kupumua.