PAKISTAN

Ujumbe wa Taliban wakutana kwa mazungumzo na serikali ya Islamabad

Kundi la Taliban
Kundi la Taliban Reuters

Waziri wa mambo ya nje wa Pakistani amepokea ujumbe wa Taliban huko Islamabad leo Jumatano, siku chache baada ya kusitishwa kwa mazungumzo ya amani kati ya wanamgambo wa Kiisilamu na serikali ya Afghanistan, serikali imesema.

Matangazo ya kibiashara

Mapumziko haya ya wiki tatu yatawezesha wajumbe kutoka pande mbili kufanya mashauriano.

Ujumbe wa Taliban, unaongozwa na Mullah Abdul Ghani Baradar, kiongozi wa kisiasa wa kundi hilo,iko Islamabad kwa siku tatu na anatarajiwa kukutana kwa mazungumzo mengine, hasa na Waziri Mkuu Imran Khan.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Pakistan Shah Mehmood Qureshi amekaribisha makubaliano kuhusu utaratibu wa mazungumzo yaliyofikiwa hivi karibuni kati ya serikali ya Kabul na Taliban, wizara yake imeripoti.

"Amani nchini Afghanistan ni muhimu kwa amani na utulivu katika kanda nzima," amesema.

Kulingana na wawakilishi wao kutoka pande hizo mbili huko Doha, ujumbe wa Taliban pia unatarajiwa kukutana na viongozi wa kundi hilo nchini Pakistan.

Viongozi hao walikuwa walikwenda mwezi nchini Pakistan mwezi Agosti, kabla ya kuanza kwa mazungumzo ya Doha.