CHINA-WHO

WHO kutuma wanasayansi wake kwenye mji wa Wuhani, China

Wataalamu wa afya wa China kwenye mji wa Hubei.
Wataalamu wa afya wa China kwenye mji wa Hubei. RFI/Stéphane Lagarde

Ujumbe wa kimataifa wa kuchunguza asili ya janga la COVID-19 utazuru China mapema mwezi Januari, Shirika la Afya Duniani, (WHO) limetangaza leo Alhamisi.

Matangazo ya kibiashara

Awali mamlaka ya China ilipinga vikali ombi la uchunguzi wa kimataifa kuhusu kujuwa asili ya virusi vya Corona , ikiona kuwa ni uchokozi, lakini imeendelea kuomba kufanyike uchunguzi wa WHO.

 

Bado haijulikani wazi ikiwa wachunguzi wa Shirika la Afya Duniani, (WHO) watasafiri kwenda Wuhan, ambapo virusi hivyo viligunduliwa kwa mara ya kwanza.

 

"WHO inawasiliana na China na inajadili ziara ya ujumbe wa kimataifa kwenda nchini humo," Babatunde Olowokure, mkuu wa dharura katika kanda ya Magharibi mwa Pasifiki, amesema katika mkutano na waandishi wa habari.

 

"Kwa sasa, inaonekana kuwa China iko tayari kupokea ujumbe, kwa kile tunachojuwa, ujumbe ambao unatarajia kwenda huko mapema mwezi Januari," ameongeza.

 

Marekani, ambayo iliishutumu China kwa kuficha ukumbwa cha janga hilo, ilitaka uchunguzi wa "uwazi" chini ya usimamizi wa WHO na kukosoa masharti yake, ambayo yaliwezesha wanasayansi wa China fkuanya awamu ya kwanza ya utafiti wa awali.

 

Televisheni ya umma ya China imebaini kwamba virusi vya Corona vilikuepo katika nchi za kigeni kabla ya kugunduliwa huko Wuhan, ikisema uwepo wake uligunduliwa kwenye vifurushi vya bidhaa zilizohifadhiwa na kwambaripoti za kisayansi zilibaini kwamba virusi vilikuwa vikisambaa barani Ulaya mwaka jana.

 

Babatunde Olowokure amesema tarehe sahihi ambayo ujumbe huo utazuru China itategemea "matokeo ya mfululizo wa vipimo vya awali," bila kutoa maelezo zaidi.