AFGHANISTAN

Watoto kumi na tano waangamia katika mlipuko mashariki mwa Afghanistan

Baadhi ya milipuko iliyotokea mjini Kabul
Baadhi ya milipuko iliyotokea mjini Kabul Najiba NOORI / AFP

Watoto kumi na watano wamepoteza maisha huku wengine Ishirini wakijeruhiwa katika mlipuko uliotokea siku ya Ijumaa  katika mkoa wa Ghazni mashariki mwa Afghanistan.

Matangazo ya kibiashara

Mlipuko huo ulitokea karibu na eneo ambapo watu walikuwa wamekusanyika katika mkoa huo, ambao unaendelea kukumbwa na ghasia licha ya mazungumzo ya amani kati ya Taliban na ujumbe uliotumwa kutoka Kabul.

Baiskeli ya magurudumu matatu iliyotegwa vilipu ambayo ilikuwa imeegeshwa mita chache kutoka kwa nyumba ambapo watu kadhaa, ikiwa ni pamoja na watoto kadhaa, walikuwa wamekusanyika.

Sherehe ya kidini ilikuwa ikiendelea. Kulingana na waandishi wa habari nchini Afghanistan, mashindano ya usomaji wa Quran yalikuwa yakifanyika wakati mlipuko ulitokea.

Mamlaka nchi humo zinasema mlipuko huo ulitokea katika wilaya inayodhibitiwa na Taliban. Ni vigumu kujua ikiwa vilipuzi hivyo vililipuliwa kwa makusudi au ikiwa vililipuliwa kimakosa.

Hata hivyo hakuna pande yoyote ambayo imedai kuhusika na mlipuko huo.