CHINA-UINGEREZA

China yasitisha safari za ndege za moja kwa moja na Uingereza

Shirika la ndege nchini Uingereza
Shirika la ndege nchini Uingereza REUTERS/Hannah McKay/File Photo

China imeamua kusitisha kwa muda usiojulikana zake za ndege za moja kwa moja kwenda na kutoka Uingereza baada ya nchi hiyo kukumbwa na aina mpya ya kirusi cha corona, msemaji wa Wizara ya Mambo ya nje.

Matangazo ya kibiashara

Kwa sasa kuna ndege nane za kila wiki kati ya nchi hizi mbili, kulingana na takwimu kutoka mamlaka ya usafiri wa anganchini Japan.

Shirika la ndege nchini Uingereza, linafanya safari mara mbili kwa wiki kati ya London na Shanghai.

Wakati huo huo mataifa kadhaa ya Ulaya tangu jana Jumatano yameanza kulegeza marufuku ya safari yaliyokuwa yameiwekea Uingereza katika juhudi za kukabiliana na kuenea kwa aina mpya ya kirusi cha Corona wakati maafisa wa Shirika la Afya Ulimwenguni, WHO wakitazamiwa kulijadili suala hilo.

Kirusi kipya cha Corona kimeikumba Uingereza na kuibua wasiwasi duniani kote wakati chanjo ya COVID-19 ikianza kutolewa.

Lakini Halmashauri Kuu ya Ulaya imeyataka mataifa ya Ulaya kuondoa marufuku ya safari iliyowekwa dhidi ya Uingereza katika siku za hivi karibuni.

Ufaransa imeanza kuifungua mipaka yake na Uingereza tangu jana Jumatano, ingawa vipimo kwa ajili ya COVID-19 vitahitajika.