JAPAN-SIASA

Japan:Waziri Mkuu wa zamani Shinzo Abe kuitwa Bungeni

Shinzo Abe Waziri Mkuu wa zamani wa Japan
Shinzo Abe Waziri Mkuu wa zamani wa Japan AP/Kyodo News

Waziri Mkuu wa zamani wa Japani Shinzo Abe anaweza kuitishwa bungeni wakati wowote kuelezea mwenyewe kuhusu uwezekano wa ukiukaji wa sheria kuhusu ufadhili wa kisiasa, vyanzo kadhaa katika serikali na chama tawala vimebaini kulingana na shirika la habari la REUTERS.

Matangazo ya kibiashara

Maandalizi yanafanywa kwa Shinzo Abe kuitishwa Ijumaa mbele ya bunge kuhojiwa na kamati kadhaa, vyanzo vimesema, na kuongeza kuwa kuna uwezekano wa kurusha moja kwa moja tukio hilo kwenye wavuti ili raia waweze kufuata kwa karibu tukio lenyewe.

Shinzo Abe, ambaye alijiuzulu mwezi Septemba mwaka huu akitoa sababu za kiafya, anatuhumiwa kufadhili chakula cha jioni kwa wafuasi wake kupitia huduma zake, kwa kukiuka sheria kuhusu ufadhili wa kisiasa.

Alipohojiwa katika Bunge mwaka jana, alikanusha madai hayo.

Kulingana na ripoti za vyombo vya habari vya nchini Japani, Shinzo Abe aliripoti kwa hiari yake siku ya Jumatatu kujibu maswali ya waendesha mashtaka wa Tokyo na alikanusha kuhusika kwa na tuhuma hizo.

Kiongozi huyo wa zamani wa serikali nchini Japani anatarajia kuzungumza na waandishi wa habari leo Alhamisi, shirika la habari la Jiji limeripoti, bila hata hivyo kutaja vyanzo.

Kesi hiyo inaweza kumuweka hatari Waziri Mkuu wa sasa, Yoshihide Suga, ambaye alikuwa shirika wa karibu wa Shinzo Abe kwa miaka nane na kumtetea bungeni.