SINGAPORE

Singapore yarekodi kisa kimoja cha aina mpya ya kirusi cha Corona

Upimaji wa virusi vya Covid 19
Upimaji wa virusi vya Covid 19 REUTERS/Alexandre Meneghini

Singapore inasemaimegundua kesi ya kwanza ya aina mpya ya kirusi cha Corona iliyogunduliwa nchini Uingereza, wakati vipimo vya awali vilivyofanywa kwa watu wengine 11 ambao tayari walikuwa wamewekwa karantini vinaonyesha uwepo wa aina mpya ya SARS-CoV -2.

Matangazo ya kibiashara

Watu hawa wote, kutoka Ulaya, wamewekwa karantini kwa siku 14 katika vituo vilivyotengwa, mamlaka nchini Singapore imesema.

"Kwa sasa hakuna ushahidi kwamba aina hii mpya kirusi cha Corona inaendelea kusambaa nchini Singapore," Wizara ya Afya ilisema Jumatano jioni.

Mtu huyo aliyeambukizwa aina mpya ya kirusi cha Corona aliwasili Singapore kutoka Uingereza mnamo Desemba 6. Aliwekwa karantini wakati alipowasili, na alipatikana na kirusi hicho mnamo Desemba 8.

Singapore imezuia wasafiri ambao hivi karibuni walisafiri kwenda Uingereza ili kuzuia kuenea kwa aina mpya ya kirusi cha Corona.