JAPAN-CORONA-AFYA

Covid 19: Karibu visa vipya 1,000 vyathibitishwa Tokyo

Maafisa wa afya nchini Japan
Maafisa wa afya nchini Japan Philip FONG / AFP

Mamlaka huko Tokyo, nchini Japan imeripoti rekodi ya maambukizi ya kila siku ya visa 949 vilivyogunduliwa katika mji mkuu wa Japani katika muda wa saa 24 zilizopita.

Matangazo ya kibiashara

Siku ya Ijumaa Japani iliripoti visa vya kwanza katika nchi hii inayokumbwa na maambukizi ya aina mpya ya COVID-19 iliyogunduliwa hivi karibuni nchini Uingereza na ambayo inaweza kuambukiza zaidi.

Nchi kadhaa imeamua kusitisha safari za ndege kutoka na kuelekea nchini Uingereza na Afrika Kusini.

Shirika la Afya Duniani, WHO, wiki hii lilikutana kwa dharura katika juhudi za kupambana na kuenea kwa aina mpya ya kirusi cha Corona, huku mataifa ya Ulaya yakitarajiwa kuanza chanjo dhidi ya Covid-19 ifikapo Jumapili ijayo.