URUSI

Covid 19: Visa vya COVID-19 vyapindukia zaidi ya milioni moja Urusi

Watalaam wa afya nchini Urusi
Watalaam wa afya nchini Urusi Sofya Sandurskaya/Moscow News Agency/Handout via REUTERS

Urusi imepitisha kizingiti cha visa milioni tatu vya maambukizi ya virusi vya Corona kwa mara ya kwanza Jumamosi.

Matangazo ya kibiashara

Takwimu rasmi zimebaini kwamba kesi mpya 29,258 zimethibitishwa na vifo vipya 567 vimeripotiwa katika muda wa saa 24 zilizopita, na kufanya idadi ya maambukizi kufikia 3,021,964.

Jumamosi Urusi pia imeidhinisha chanjo yake kuu dhidi ya COVID-19, Sputnik V,  kwa watu wenye umri wa zaidi ya miaka 60, vyombo vya habari vya Urusi vimripoti vikinukuu wizara ya afya.

Watu zaidi ya 60 waliondolewa kwenye mpango wa chanjo hiyo nchini Urusi.