CHINA

Covid 19: Visa vipya 21 vya maambukizi vyarekodiwa China

Maafisa wa afya jijini Beijing wakipima kiwango cha joto katika vita dhidi ya Corona
Maafisa wa afya jijini Beijing wakipima kiwango cha joto katika vita dhidi ya Corona AFP

China imerekodi visa vipya 21 vilivyothibitishwa vya maambukizi ya virusi vya Corona katika muda wa saa ishirini na nne zilizopita, mamlaka ya afya imeripoti leo Jumatatu.

Matangazo ya kibiashara

Katika taarifa, Tume ya Kitaifa ya Afya imesema visa 15 vinahusu watu waliowasili nchini humo wakitokea katika nchi za kigeninje.

Kulingana na takwimu za Tume ya kitaifa ya Afya, visa 86,976 vya maambukizi ya virusi vya Corona vimethibitishwa katika China bara.

Janga la COVID-19 limesababisha vifo vya watu 4,634 nchini China. Hakuna vifo vipya vilivyoripotiwa leo Jumatatu, kulingana na mamlaka ya afya.