URUSI

Visa vipya 27,787 vyathibitishwa katika muda wa saa 24 Urusi

Maafisa wa afya nchini Urusi wakifanya vipimo vya Covid 19
Maafisa wa afya nchini Urusi wakifanya vipimo vya Covid 19 REUTERS/Stringer

Urusi imerekodi visa vipya 27,787 vya maambukizi ya virusi vya Corona katika muda wa saa 24 zilizopita, ikiwa ni pamoja na visa 6,253 huko Moscow, na kufanya jumla ya visa 3,078,035 katika nchi nzima tangu kuzuka kwa janga hilo.

Matangazo ya kibiashara

Mamlaka nchi humo pia imeripoti vifo vipya 487 kwa jumla ya vifo 55,265 vilivyorekodiwa tangu kuzuka kwa mgogoro huyo wa kiafya.

Mlipuko wa virusi vya Corona unaosababisha ugonjwa wa COVID-19, ulitokea katika mkoa wa Hubei nchini China mwishoni mwa mwaka 2019.

Kufikia sasa kinachojulikana ni kuwa COVID-19, ni ugonjwa ambao unaothiri mfumo wa kupumua wa binadamu.

Dalili zake ni pamoja na homa kali, kukohoa ambako baada ya wiki moja muathiriwa anakabiliwa na tatizo la kupumua.