CHINA

Zhang Zhan ahukumiwa kifungo cha miaka minne kwa kuripoti janga la Corona

Abiria wakiwa wamevalia barakoa nchini China
Abiria wakiwa wamevalia barakoa nchini China REUTERS/Stringer

Mwandishi wa habari Zhang Zhan amehukumiwa kifungo cha miaka minne kwa kuripoti mlipuko wa kwanza wa virusi vya Corona katika mji wa Wuhan. Hukumu hiyo imetolewa na mahakama ya Shanghai.

Matangazo ya kibiashara

Mahakama ya Shanghai imechukua uamuzi kifungo cha miaka minee dhidi ya mwandishi wa habari Zhang Zhan baada ya kuangazia mlipuko wa kwanza wa virusi vya Corona, amesema mwanasheria wake.

Kwa mujibu wa mashataka yanayomkabili, alisafiri hadi Wuhan mwezi Februari kuripoti kuhusu mlipuko wa virusi bila kuzingatia kanuni zilizowekwa.

Ripoti yake aliyoweka mubashara katika mtandao wa kijamii ilivuma sana mwezi Februari, ilimweka mashakani baada ya kuvutia mamlaka za China.

Kesi yake, ambayo imefunguliwa Jumatatu hii, ilichukua saa chache kbala ya kutolewa uamuzi. Mwandishi huyo wa habari, mwenye umri wa miaka 37, alikamatwa mwezi Mei mwaka huu, akishumiwa "kuchochea vurugu" kwa kueneza "habari za uwongo". Shtaka linalotumiwa mara kwa mara dhidi ya wapinzani wa serikali.

Bi. Zhang ni mmoja wa wanahabari kadhaa raia wa China waliojipata mashakani kwa kuripoti kuhusu mwenendo wa virusi vya corona katika eneo la Wuhan.

Wakili huyo wa zamani aliye na umri wa miaka 37 aliyezuiiwa mwezi Mei, amegoma kula kwa miezi kadhaa. Mawakili wake wanasema afya yake imedhoofika vibaya.