JAPAN

Japan: Suga kutangaza hali ya dharura kwa mji wa Tokyo

Yoshihide Suga Waziri Mkuu wa Japan
Yoshihide Suga Waziri Mkuu wa Japan Kimimasa Mayama/Pool via REUTERS

Waziri Mkuu wa Japani Yoshihide Suga amesema leo Jumatatu kwamba serikali imepanga kutangaza hali ya dharura kwa mji mkuu wa nchi hiyo, Tokyo, na viunga vyake.

Matangazo ya kibiashara

Idadi ya visa vipya vya maambukizi ya virusi vya Corona inaendelea kuongezeka nchini Japani na kuweka shinikizo kwa mfumo wa afya.

Rekodi mpya ya visa 4,520 imerekodiwa siku ya Alhamisi, Desemba 31, pamoja na zaidi ya visa 1,300 vya maambukizi katika mji mkuu Tokyo. Viongozi wana hofu ya kuzuka mlipuko mpya wa virusi vya Corona na kuitaka mamlaka katika mji mkuu kuomba serikali kutangaza hali ya hatari.

Yoshihide Suga hadi sasa amesita kutangaza hali ya dharura, akiwa na wasiwasi juu ya uwezekano wa kutokea mdororo wa uchumi.

Katika jaribio la kuzuia kuenea kwa virusi, mikahawa na baa huko Tokyo sasa italazimika kufungwa saa mbili usiku mchana, badala ya saa nne usiku 10 hapo awali, wakati maduka ya kuuza pombe yatalazimika kufungwa saa moja usiku.