KOREA KUSINI

Korea Kusini yapiga marufuku mikusanyiko nchi nzima

Mhudumu wa afya akiendelea na kazi ya kutoa huduma kwa mgonjwa
Mhudumu wa afya akiendelea na kazi ya kutoa huduma kwa mgonjwa REUTERS

Marufuku ya mikusanyiko katika mji mkuu wa Korea Kusini, Seoul, kupambana na mlipuko wa Corona imeongezwa muda na kwa sasa hatua hiyo itahusu nchi nzima, serikali imesema leo Jumatatu.

Matangazo ya kibiashara

Korea Kusini imeendelea kushuhudia ongezeko la visa vipya vya maambukizi ya virusi vya Corona, na kusababisha raia nchini humo kuwa na wasiwasi mkubwa.

Mikusanyiko ya zaidi ya watu wanne imepigwa marufuku huko Seoul na viunga vyake tangu Desemba 23.

Hatua hii hapo awali ilitarajiwa kumalizika mnamo Januari 3 lakini iliongezwa muda, sawa na sheria kali za watu kutokaribiana zinazolenga mikahawa, makanisa na vituo sehemu za burudani.

Kampeni ya kitaifa ya chanjo inatarajiwa kuanza mwezi Februari.