HONG KONG-SIASA-DEMOKRASIA

Wapinzani kadhaa wakamatwa chini ya sheria ya usalama

Wanaharakati wakati wa maandamano yaliyopita katika eneo la Hong Kong
Wanaharakati wakati wa maandamano yaliyopita katika eneo la Hong Kong AFP/Anthony Wallace

Polisi ya Hong Kong imesema leo Jumatano kuwa imewakamata watu 53 katika operesheni isiyokuwa ya kawaida dhidi ya maandamano ya wanaharakati wanatetea demokrasia katika eneo hilo tangu China kutangaza sheria ya usalama katika jimbo la Hong Kong.

Matangazo ya kibiashara

Operesheni hii iliyoanza alfajiri inaonekana kuwa imefanyika kufuatia uchaguzi usiyo rasmi uliofanyika mwezi Julai na wapinzani ili kuteua wagombea wa uchaguzi wa wabunge, ambao uliahirishwa.

Msako wa polisi ulifanyika katika nyumba sabini, vyanzo vya polisi vimebaini. Kulingana na vyombo vya habari katika eneo hilo, majengo ya taasisi ya uchunguzi kuhusiana na uchaguzi, ofisi moja ya mawakili na majengo vinakofanyia kazi vyombo kadhaa vya habari - Apple Daily, Stand News na Immediahk - yalifanyiwa msako kama huo.

Waziri wa usalama wa Hong Kong amethibitisha kukamatwa kwa watu kadhaa wanaoshukiwa kutaka "kupindua" serikali ya eneo hilo. John Lee, akizungumza bungeni, amesema mamlaka hazitavumilia kitendo chochote cha "uasi".