INDONESIA

Indonesia yapata kisanduku cheusi cha ndege ya shirika la Sriwijaya Air

Maafisa wa uokoaji nchini Indonesia wakitoa mabaki ya ndege iliyoanguka baharini Januari 10 2021
Maafisa wa uokoaji nchini Indonesia wakitoa mabaki ya ndege iliyoanguka baharini Januari 10 2021 © Adek Berry / AFP

Mamlaka nchini Indonesia imetangaza kwamba imepata kisanduku kimoja cheusi cha ndege ya shirika la ndege la Sriwijaya Air ambayo ilianguka katika Bahari ya Java siku ya Jumamosi, msemaji wa jeshi la majini amesema Jumanne.

Matangazo ya kibiashara

Kisanduku cheusi kilisafirishwa katika bandari ya Jakarta, msemaji Fajar Tri Rohadi aameluambia shirika la habari la REUTERS.

Kulingana na Waziri wa Uchukuzi, Budi Karya Sumadi, kisanduku hiki cheusi ni kisanduku cha kuhifadhia data.

Boeing 737-500 ya shirika la ndege la Sriwijaya Air, iliyokuwa imebeba watu 62 wakiwemo wahudumu 12, ilianguka dakika nne baada ya kuruka kutoka uwanja wa ndege mkukuu huko Jakarta.

Ndege hiyo ilipaswa kufika Pontianak, mji mkuu wa jimbo la Kalimantan Magharibi, kwenye kisiwa cha Borneo, wakati ngege hiyo ilipoppteza mawasiliano na maafisa wanao.

Miili ya watu waliokuwemo katika ndege hiyo imepatikana katika eneo la tukio Jumanne, pamoja na vitu mbalimbali vya abiria kama vile pochi zilizo na vitambulisho.

Hili ni janga kubwa la kwanza la usafiri wa anga nchini Indonesia tangu ajali ya ndege ya shirika la ndege la Boeing 737 MAX iliyoua watu 189 mnamo mwaka 2018.

Boeing 737 ambayo ilianguka katika Bahari ya Java, hata hivyo, ilikuwa ya muundo tofauti.

Baada ya data za ndege na rekodi za sauti za chumba cha ndege kupatikana, Kamati ya Kitaifa ya Usalama ya Usafirishaji (KNKT) imebaini kwamba inaweza kufafanua habari iliyokusanywa ndani ya siku tatu.