CHINA

COVID-19: China yatangaza kifo cha kwanza katika kipindi cha miezi nane

Upimaji wa Corona nchini China
Upimaji wa Corona nchini China AFP

China imerekodi idadi kubwa zaidi ya kila siku ya visa vilivyothibitishwa vya maambukizi ya virusi vya Corona tangu zaidi ya miezi kumi, wakati visa vya mambukizi katika mkoa wa kaskazini mashariki mwa nchi hiyo vimeongezeka mara tatu, na hivyo kuwa tishio la afya linalozidi kuongezeka nchini China.

Matangazo ya kibiashara

Katika Jarida lake la kila siku kuhusu janga hilo, Tume ya kitaifa ya afya pia imebaini kwamba imerekodi kifo kipya kilichosababishwa na ugonjwa COVID-19, ikiwa ni kifo cha kwanza kutokea nchini humo tangu mwezi Mei mwaka uliyopita.

Kwa muda wa saa ishirini na nne zilizopita, mamlaka ya afya imerekodi maambukizi mapya 138, wakati visa 115 vya maambukizi vilithibitishwa siku moja iliyopita na hivyo kuonyesha rekodi tangu Machi 5, 2020.

Tume imesema visa 124 kati ya visa hivi vipya ni raia wa China. Wakati huo huo maambukizi 81 yameripotiwa katika Mkoa wa Hebei, ambao unapakana na mji mkuu Beijing, na visa 43 vya maambukizi vimeripotiwa katika Mkoa wa Heilongjiang kaskazini mashariki.

Ikiwa ripoti za kila siku za hivi karibuni zinaendelea kuwa chini kuliko zile zilizoripotiwa wakati janga hilo lilipokuwa baya zaidi, mwanzoni mwa mwaka 2020, mamlaka nchini China mwezi huu ilipiga mlarufuku zaidi ya wakazi milioni 28 kusalia majumbani kwao kama sehemu ya hatua kali zilizokusudiwa kukomesha kuenea kwa virusi.

Kuongezeka kwa maambukizi mapya kunakuja kabla ya likizo ya Mwaka Mpya wa Lunar, mwezi ujao, wakati mamia ya mamilioni ya watu wamezoea kusafiri. Hata hivyo, baadhi ya mikoa tayari imehimiza wakaazi wao kutosafiri.

Kulingana na takwimu kutoka Tume ya kitaifa ya Afya, idadi ya visa vya maambukizi katika China bara imefikia 87,844 na vifo 4,635.