INDONESIA

Watu zaidi ya 30 wapoteza maisha kufuatia tetemeko la ardhi

Madhara yaliyojitokeza nchini Indonesia
Madhara yaliyojitokeza nchini Indonesia Reuters/Adi Kurniawan

Waokoaji nchini Indonesia, wanawatafuta watu kwenye vifusi vya majengo yaliyoporomoka baada ya kutokea kwa tetemeko la ardhi katika kisiwa cha Sumawesi na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 30.

Matangazo ya kibiashara

Tetemeko hilo lenye ukubwa wa richa 6.2 limetokea Ijumaa asubuhi, na kusababisha mamia ya watu kujeruhiwa.

Maelfu ya watu wengine, hawana maakazi yao baada ya tetemeko hilo kusababisha hasara katika kisiwa hicho.

Kisiwa cha Sulawesi kina historia ya kutokea kwa majanga ya tetemo la ardhi na tsunami na mwaka 2018 watu zaidi ya elfu mbili walipoteza maisha baada ya majanga hayo mawili.

Mbali na makaazi ya watu kuporomoka, majengo ya serikali ikiwemo hopsitali, zimeporomoka pia.

Mwaka 2004, watu 226,000 walipoteza masiha katika kisiwa cha Sumatra baada kutokea kwa tetemeko la ardhi.