CHINA

Covid 19: Visa 109 vipya vyaripotiwa China

Maafisa wa afya nchini China
Maafisa wa afya nchini China Greg Baker / AFP

China imerekodi visa vipya 109 vilivyothibitishwa vya maambukizi ya virusi vya Corona katika muda wa saa ishirini na nne zilizopita, idadi ambayo ni sawa na ile iliyorekodiwa siku moja iliyopita, mamlaka ya afya imebaini leo Jumatatu.

Matangazo ya kibiashara

Katika taarifa yake, Tume ya kitaifa ya Afya imebaini kwamba imerekodi visa 93 vya maambukizi kutoka ndani ya nchi, ikiwa ni pamoja na idadi kubwa (54) katika mkoa wa Hebei, ambao unapakana na mji mkuu wa Beijing.

Kulingana na takwimu za tume hiyo, visa 89,336 vya maambukizi vimethibitishwa katika China Bara.

Hakuna vifo vya vipya vilivyorekodiwa. Idadi ya vifo kutokana na virusi vya Corona nchi kote imefikia
4,635.