INDONESIA

Idadi ya vifo Indonesia yaongezeka hadi 78

Madhara nchini Indonesia baada ya tetemeko la ardhi
Madhara nchini Indonesia baada ya tetemeko la ardhi Antara Foto/Dhemas Reviyanto/ via REUTERS

Waokoaji nchini Indonesia wamepata miili zaidi kwenye vifusi vya majengo vilivyoharibiwa na tetemeko kubwa la ardhi na kufikisha idadi ya vifo 78, huku wanajeshi wakiendelea kufungua barabara kufanikisha kupatikana kwa chakula cha msaada.

Matangazo ya kibiashara

Tetemeko lenye uzito wa 6.2 kwa kipimo cha Richter  liliathiri mji wa Mamuju na Majene katika kisiwa cha Sulawesi, watu 67 wakiripotiwa kufa katika mji wa Mamuju na 11 katika mji wa Majene.

Huduma za umeme na mawasiliano zimeanza kurejea, maelfu ya watu wakiachwa bila makaazi na 800 wakipata majeraha.

Kisiwa cha Sulawesi kina historia ya kutokea kwa majanga ya tetemo la ardhi na tsunami na mwaka 2018 watu zaidi ya elfu mbili walipoteza maisha baada ya majanga hayo mawili.

Mbali na makaazi ya watu kuporomoka, majengo ya serikali ikiwemo hospiitali, ziliporomoka pia.

Mwaka 2004, watu 226,000 walipoteza masiha katika kisiwa cha Sumatra baada kutokea kwa tetemeko la ardhi.