SRI LANKA

Sri Lanka kuchunguza mashtaka ya uhalifu wa kivita

Mwanajeshi wa Sri Lanka akiwa jijini Colombo
Mwanajeshi wa Sri Lanka akiwa jijini Colombo REUTERS/Athit Perawongmetha

Sri Lanka imetangaza kuanzisha uchunguzi kuhusu madai ya uhalifu wa kivita uliofanywa na askari wake wakati wa mmapigano na Tamil Tigers, mwezi mmoja kabla ya mkutano wa Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa, ikiwa ni rekodi ya haki za binadamu katika nchi hii.

Matangazo ya kibiashara

Kwa miaka 37, Sri Lanka imekuwa iliathiriwa na mapigano makali kati ya vikosi vya serikali na wapiganaji wa Tamil Tigers, ambayo yalisababisha vifo vya zaidi ya watu 100,000. Mzozo ulimalizika mwezi Mei 2009 baada ya waaasi wa Tamil Tigers kuangamizwa, katika utawala wa Mahinda Rajapaksa.

Wanaharakati wa haki za binadamu wanashutumu vikosi vya Sri Lanka kwa kuua raia wasiopungua 40,000 wa Kitamil wakati wa miezi ya mwisho ya vita. Mashtaka haya yamekataliwa na serikali zinazofuatana mamlakani.

Siku ya Ijumaa rais Gotabaya Rajapaksa aliteua tume ya kuchunguza uchunguzi wa serikali zilizopita, ofisi yake imesema.

Tume hii ina miezi sita kuchunguza tuhuma za "ukiukaji wa haki za binadamu" na "ukiukaji mkubwa wa sheria za kimataifa za kibinadamu", kulingana na chanzo hicho. Pia imepewa jukumu la kuchunguza "uchunguzi uliotangulia ambao haukuhitimishwa" uliozinduliwa na Colombo kufuatia shinikizo la kimataifa.

Ikijibu kwenye ukurasa wake Twitter kuhusu tangazo hilo, shirika la kimataifa la haki za binadamu la Amnesty International limesema kwamba "Sri Lanka ina historia ndefu ya tume za uchunguzi ambazo hazijawahi kufanikiwa kwa kutenda haki au kupatanisha waathiriwa wa ukiukaji wa haki za binadamu."

Amnesty International imetoa wito kwa shirika la Umoja w Mataifa linalohudumia wakimbizi (UNHCR) kuanzisha mchakato mpya dhidi ya Sri Lanka ili kuhakikisha haki kwa wahanga wa vita.