MYANMAR

Licha ya kuwa hawajulikani walipo, Suu Kyi na viongozi wengine washtakiwa,

Kiongozi wa Myanmar, Aung San Suu Kyi, ambaye sasa anashikiliwa na jeshi.
Kiongozi wa Myanmar, Aung San Suu Kyi, ambaye sasa anashikiliwa na jeshi. REUTERS/Ann Wang

Polisi nchini Myanmar, imemfungulia mashtaka kadhaa kiongozi wa kiraia Aung San Suu Kyi, hatua inayokuja baada ya wanajeshi kufanya mapinduzi.

Matangazo ya kibiashara

Suu Kyi, sasa ataendelea kuzuiliwa hadi Februari 15 hii ni baada ya kuvuja kwa hati ya mashtaka ya polisi.

Mashtaka aliyofunguliwa ni pamoja na kukiuka sheria za manunuzi, pamoja na kukutwa na vifaa vya mawasiliano.

Hata hivyo hadi sasa haifahamiki Suu Kyi anazuiliwa katika jela gani, lakini taarifa zinasema huenda akawa anazuiliwa nyumbani kwake, mjini Nay Pyi Taw.

Rais aliyepinduliwa Win Myint, pia anaendelea kuzuiliwa na yeye amefunguliwa mashtaka ya kukiuka sheria ya kuzuia mikusanyiko ya watu wakati wa janga la Corona.

Tangu wapinduliwe, si rais Myint wala Suu Kyi wamezungumza na uma.

Mapinduzi hayo yaliyoongozwa na mkuu wa majeshi Min Aung Hlang, ameteua wanajeshi wengine 11 kuongoza Serikali kwa kipindi cha mwaka mmoja.

Jeshi linatetea hatua yake kwa kile inachodai ni uchaguzi wa mwaka jana ulikuwa na dosari, uchaguzi ambao ulishuhudia chama cha Suu Kyi kikipata ushindi mkubwa dhidi ya vyama vinayowaunga mkono wanajeshi.

Katika hatua nyingine, nchi ya China imetumia kura ya turufu kuzuia azimio la umoja wa Mataifa kuhusu kulaani mapinduzi hayo ya kijeshi.