SAUDI ARABIA - AHMED ZAKI YAMANI

Waziri wa muda mrefu wa Nishati wa Saudi Arabia, Ahmed Zaki Yamani afariki.

Daidaikun Musulmin da suka samu damar gudanar da Sallar Idi karama a Masallacin Harami dake birnin Makkah.
Daidaikun Musulmin da suka samu damar gudanar da Sallar Idi karama a Masallacin Harami dake birnin Makkah. AFP

Ahmed Zaki Yamani, aliyekuwa waziri wa muda wa mrefu wa nishati nchini Saudi Arabia, na ambaye alikuwa mstari wa mbele kutatua mzozo wa mafuta wa mwaka 1973 nchini humo amefariki akiwa na umri 90, jijini London Uingereza.

Matangazo ya kibiashara

Runinga ya taifa ya Saudi Arabia, imetangaza kifo cha Yamani, na kuongeza kuwa atazikwa katika jiji la Mecca.

Yamani alizaliwa  kule mecca mwaka 1930, babake alikuwa mwalimu wa dini na wakili wa Waislamu.

Yamani alipata mafunzo katika vyuo vikuu vya Harvard na kile cha New York.

Kadhalika atakumbukwa kwa kuongoza taifa lake kuwa mstari wa mbele katika soko la mafuta, miongoni mwa mataifa yanayouza mafuta duniani yaani, Organization of the Petroleum Exporting Countries (OPEC).

Wakati aliyekuwa rais wa Marekani, Richard Nixon, alipoanza kuunga mkono Isreal  ndani ya OPEC, mataifa ya kiarabu yakiongozwa na Saudi Arabia, yalikubaliana kupunguza mchango wao kwa asilimia 5 kila mwezi, na baada ya Nixon kuzindisha msimamo wake kwa Israeli, ndipo muungano wa “oil weapon” ulizaliwa

Yamani alishikilia wadhifa wa waziri wa nishati kuanzia mwaka 1962 hadi mwaka 1986.