CHINA-UCHUMI

Xi Jinping adai "ushindi kamili" dhidi ya umaskini nchini China

Rais wa China Xi Jinping.
Rais wa China Xi Jinping. STR AFP/File

Siku chache kabla ya mkutano wa wajumbe wa Chama cha Kikomunisti huko Beijing, rais wa China Xi Jinping ametangaza kwamba China imepata imefaulu kuubwaga umasikini, huku akitaja mafanikio hayo kuwa ni "muujiza".

Matangazo ya kibiashara

Umaskini umekuwa ukiripotiwa zaidi katika mkoa wa Kusini wa Guangxi na huko Dongbei, kaskazini mashariki mwa China. Kwa upande wa viongozi wa China, wanasema lengo la kutokomeza umasikini kabisa lilifanikiwa mwaka jana kote nchini. Kwa nini mwaka jana? Kwa sababu mafanikio hayo yalitakiwa kuja kabla ya maadhimisho ya miaka mia moja ya chama tawala katika msimu huu wa joto, mnamo mwezi Julai

Kulingana na Benki ya Dunia, zaidi ya Wachina milioni 800 wametoka kwenye umaskini tangu kufunguliwa kwa uchumi mwishoni mwa miaka ya 70. "Ushindi kamili" uliokaribishwa wakati wa hafla na sherehe kubwa katika makao makuu ya Bunge na Xi Jinping ambaye alikuwa amefanya sula hilo kuwa moja ya vipaumbele vyake, na vita dhidi ya ufisadi:

"Leo, tunaweza kutangaza kwamba kutokana na juhudi za pamoja za raia na chama [...], nchi yetu imeibuka ushindi wa dunia katika vita dhidi ya umaskini. [...] Karibu watu milioni 100 wa vijijini, vijiji 128,000 katika kaunti 832 vimeondokana na umaskini uliokithiri. [...] Huu ni muujiza wa kibinadamu ambapo utakumukwa kihistoria. "

Muujiza ambao hakuna nchi nyingine imeweza kutimiza kwa muda mfupi sana, rais wa China amesema, akionyesha ubora wa mfano unaodhaniwa kuwa unaweza kusaidia nchi zingine.

Katika miaka ya hivi karibuni afisa anayeshughulikia kupunguza umaskini katika Baraza la Serikali la China Bw. Liu Wenshu alisema "ingawa uchumi wa China unashika nafasi ya pili kwa ukubwa wake duniani, lakini bado China ilikuwa inakabiliwa na changamoto kubwa katika kupambana na umaskini, na kazi ngumu zaidi ya kujenga jamii yenye neema ilikuwa vijijini, hususan katika sehemu zinazokumbwa na umaskini".