URUSI-SIASA-HAKI

Navalny aondolewa katika jela na kupelekwa kuzuiliwa kusikojulikana

Alexei Navalny wakati wa kesi yake ikisikilizwa kuhusu kutahmini rufaa aliyokata dhidi ya uamuzi wa mahakama wa kubadili adhabu yake kuwa adhabu kamili ya kifungo jela , Moscow, Februari 20, 2021.
Alexei Navalny wakati wa kesi yake ikisikilizwa kuhusu kutahmini rufaa aliyokata dhidi ya uamuzi wa mahakama wa kubadili adhabu yake kuwa adhabu kamili ya kifungo jela , Moscow, Februari 20, 2021. REUTERS - MAXIM SHEMETOV

Mkurugenzi wa mamlaka ya magereza nchini Utusi amebthibitisha kwamba mpinzani wa kisiasa nchini Alexei Navalny amehamishwa kutoka gereza alililokuwa akizuiliwa jijini Moscow kwenda kituo kingine cha mahabusu ambapo atatumikia kifungo chake cha miaka miwili na nusu, shirika la habari la RIA limeripoti.

Matangazo ya kibiashara

Alexander Kalashnikov hakuelezea ni wapi Alexei Navalny amehamishiwa, RIA imeongeza.

Haijulikani wazi ikiwa Navalny tayari amewasili katika kituo hiki au yuko katika harakati za kuhamishwa.

Siku ya Alhamisi, wakili wa mpinzani wa rais wa Urusi Vladimir Putin alibaini kwamba Navalny alihamishiwa katika kituo cha siri kinachopatikana nje ya mji wa Moscow, mahali ambapo inaweza kuwa kambi ya wafungwa.