CHINA-AFYA

Coronavirus: Visa vipya 19 vya maambukizi vyathibitishwa China

Kulingana na watafiti wa China, masharti ya watu kutotembea na vizuizi vikali vya kiafya havitatosha kwa kudhibiti vilivyo janaga la Covid-19 mwaka 2021.
Kulingana na watafiti wa China, masharti ya watu kutotembea na vizuizi vikali vya kiafya havitatosha kwa kudhibiti vilivyo janaga la Covid-19 mwaka 2021. AP - Ng Han Guan

China imerekodi visa vipya 19 vilivyothibitishwa vyamaambukizi ya virusi vya corona katika muda wa saa ishirini na nne zilizopita, dhidi ya idadi ya visa 6 siku moja kabla, maafisa wa afya wamesema leo Jumatatu.

Matangazo ya kibiashara

Katika taarifa, tume ya kitaifa ya afya imesema watu 19 kutoka nchi za kigeni ndio walikutwa na virusi hiyo vinavyosababisha ugonjwa hatari wa COVID-19.

Kulingana na takwimu za tume hiyo, maambukizi 89,912 yamethibitishwa katika China Bara.

Hakuna vifo vipya vilivyorekodiwa leo Jumatatu. Janga la COVID-19 limesababisha vifo vya watu 4,636 nchini China.