CHINA-AFYA

Coronavirus: Visa vipya 11 vyathibitisha China

Mfanyakazi wa afya anachukua sampuli ya swab kutoka kwa mkazi katika mji wa Wuhan nchini China, ambapo wataalam wa WHO walitembelea katika kujaribu kugundua  chanzo cha virusi vya Covid-19.
Mfanyakazi wa afya anachukua sampuli ya swab kutoka kwa mkazi katika mji wa Wuhan nchini China, ambapo wataalam wa WHO walitembelea katika kujaribu kugundua chanzo cha virusi vya Covid-19. Hector RETAMAL AFP

China imerekodi visa vipya 11 vilivyothibitishwa vya maambukizi ya virusi vya Corona katika muda wa saa 24 zilizopita, dhidi ya visa 19 siku moja kabla, maafisa wa afya wamebaini leo Jumanne.

Matangazo ya kibiashara

Katika taarifa, tume ya kitaifa ya Afya imesema visa vyote vipya vinahusu watu waliowasili nchini humo wakitokea nchi za kigeni

Kulingana na takwimu za tume hiyo, maambukizi 89,923 yamethibitishwa katika China Bara.

Hakuna vifo vipya ambavyo vimeripitiwa leo Jumanne. Idadi ya vifo nchini China imefikia 4,636.