BURMA-MAREKANI-UNSC-DIPLOMASIA

Marekani kushinikiza UN kwa mazungumzo kuhusu Burma

Linda Thomas-Greenfield, mwanadiplomasia mkongwe, aliteuliwa na Joe Biden kuwa balozi wa Marekani kwenye Umoja wa Mataifa.
Linda Thomas-Greenfield, mwanadiplomasia mkongwe, aliteuliwa na Joe Biden kuwa balozi wa Marekani kwenye Umoja wa Mataifa. © Pool photo by Greg Nash

Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa Linda Thomas-Greenfield amesema anatarajia kutumia uenyekiti wa Marekani kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa mwezi huu kushinikiza "mazungumzo makubwa" zaidi  kuhusu Burma.

Matangazo ya kibiashara

Akiongea na waandishi wa habari, Linda Thomas-Greenfield ameongeza kuwa anakusudia kuandaa mazungumzo haya "haraka iwezekanavyo".

Mwezi uliopoita Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilielezea katika taarifa yake wasiwasi wake juu ya hali ya hatari ya mwaka mmoja kipindi kilichowekwa na jeshi la Burma siku ya mapinduzi mnamo Februari 1, lakini halijailaani jaribio hilo la mapinduzi kwa sababu ya upinzani kutoka Urusi na China.

Tangu jeshi la Burma kuchukuwa madaraka, na kumfunga kiongozi aliyechaguliwa kidemokrasia Aung San Suu Kyi, maandamano yameongezeka kote nchini, licha ya onyo kutoka kwa mamlaka.

Polisi, ambao hutumia gesi ya kutoa machozi na risasi za mpira kuwatawanya waandamanaji, walitumia nguvu kali siku ya Jumapili, na kuua watu 18, kulingana na Ofisi ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa.

Aung San Suu Kyi aliripoti mahakamani Jumatatu kwa mashtaka mawili mapya, wakili wake alisema. Kesi yake kuhusiana na mashitaka hayo imepangwa kusikilizwa Machi 15.

Linda Thomas-Greenfield amesema Washington ilikuwa tayari kushitikiana kimataifa "kushinikiza wanajeshi kubadili hatua zao na kurudisha serikali iliyochaguliwa kidemokrasia."

"Lakini vurugu ambazo tunaona hivi sasa hazionyeshi kuwa wako tayari kuchukua kile ninachokiona kama uamuzi rahisi kwao," ameongeza. "Kwa hivyo lazima tuongeze shinikizo."