BURMA-USALAMA-SIASA

Burma: Waandamanaji wakumbwa na mauaji mengine

Maandamano huko Mandalay,  Jumatano Machi  2021.
Maandamano huko Mandalay, Jumatano Machi 2021. AP

Vikosi vya Burma vimefyatua tena risasi za moto na kutumia mabomu ya machozi leo Jumatano (Machi 3) dhidi ya waandamanaji wanaotetea demokrasia katika miji kadhaa kote nchini.  

Matangazo ya kibiashara

Angalau watu kumi na moja wameuawa na wengi wengi wamejeruhiwa, wengine kadhaa kati yao wana hali mbaya. Wawili wameuawa karibu na mji wa Mandalay, mmoja amepigwa risasi kichwani, mwingine amepigwa risasi kifuani, ikiwa ni pamoja na msichana mdogo wa miaka 19.

Maandamano yanaendelea katika miji kadhaa kote nchini, ukiwemo mji mkuu wa uchumi wa Myanmar Yangon, ambapo watu wamefunga barabara kwa matairi na waya kuzuia polisi wasiwakaribie.

Karibu na Sule Pagoda maarufu katikati mwa mji, waandamanaji walimiminika katika eneo hilo huku wakisambaza ardhini picha za Min Aung Hlaing, jenerali anayehusika na mapinduzi, ikiwa ni mbinu ya kupunguza kasi kwa vikosi vya usalama ambao wanafanya kila liwezekanalo kuzuia kutembea juu ya picha hizi.